Zelensky ashutumu shirika la Amnesty kwa kutuhumu wanajeshi wake

Zelensky ashutumu shirika la Amnesty kwa kutuhumu wanajeshi wake

NA AFP

KYIV, UKRAINE

RAIS wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelishutumu shirika la Amnesty International kwa kudai wanajeshi wa nchi hiyo wanahatarisha maisha ya raia wanapopambana na uvamizi wa wanajeshi wa Urusi.

Shutuma hizo dhidi ya Amnesty zinajiri wakati ambapo meli nyingine tatu zilizobeba tani 58,000 za nafaka zikitarajiwa kuondoka bandari za Bahari Nyeusi – Black Sea.

Shehena hiyo ya nafaka inasafirishwa ng’ambo chini ya mkataba uliotiwa saini juzi kati ya Urusi na Ukraine kwa lengo la kupunguza uhaba wa chakula ulimwenguni.

Katika ripoti iliyotolewa Alhamisi, shirika la Amnesty liliorodhesha miji 19 mikubwa na mingine midogo ambako wanajeshi wa Ukraine walionekana kuweka hatarini maisha ya raia kwa kukita kambi zao katika maeneo ya makazi.

Lakini Rais Zelensky alitaja madai hayo kuwa sawa na “kumlaumu mwathiriwa bila sababu maalum.”

TAFSIRI: CHARLES WASONGA

  • Tags

You can share this post!

Uchaguzi kuzima nyota za wanasiasa maarufu

Sadio Mane aongoza Bayern kubomoa Frankfurt katika...

T L