Ziara ya Ruto ng’ambo yazua hisia mseto nchini

Ziara ya Ruto ng’ambo yazua hisia mseto nchini

NA BENSON MATHEKA

ZIARA ya Rais William Ruto katika nchi za Uingereza na Amerika imezua maoni mseto kutoka kwa Wakenya, baadhi wakidai angesubiri amalize kuunda serikali na wengine wakisema anatekeleza majukumu yake rasmi.

Rais Ruto yuko Uingereza kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth na kukutana na Mfalme Charles kabla ya kuelekea New York, Amerika kuhudhuria mkutano wa marais na viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Katika nchi hizo mbili, Rais Ruto anatarajiwa kukutana na maafisa wa serikali na sekta ya kibinafsi.

Hata hivyo, kuna Wakenya wanaomkosoa kwa kuwa na pupa ya kufanya ziara rasmi hata kabla ya kutaja baraza lake la mawaziri.

“Nafikiri angesubiri ili amalize kuunda serikali,” akasema David Kimani, mchanganuzi. wa siasa.

Kulingana na Bw Kioko Muteti, mkazi wa Nairobi, hakuna makosa Rais Ruto kusafiri Amerika.

“Hakuna pengo katika baraza la mawaziri kwa kuwa katiba inasema wataondoka ofisini pale wapya watakapoteuliwa. Isitoshe, mkutano wa Umoja wa Mataifa uliandaliwa hata kabla ya Rais Ruto kuingia mamlakani na kama kalenda yake inamruhusu hakuna kinachomzuia kuwakilisha maslahi ya Kenya,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Sasa koma kulaumu mahakama, Odinga afokewa na viongozi wa...

TAHARIRI: Wabunge watumikie raia kwa uaminifu

T L