Michezo

Zidane atisha kugura Real isipomkubali mwanawe kuwa kipa

May 19th, 2019 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

KOCHA Zinedine Zidane ameonya Real Madrid hatasita kujiuzulu kwa mara ya pili ikiwa waajiri hawa wake wataingilia shughuli yake ya kuchagua kikosi, tovuti ya Sportstar ilidai Mei 18, 2019.

Ripoti nchini Uhispania zinasema kwamba Mfaransa Zidane yuko tayari kumfanya mtoto wake wa kiume Luca kuwa kipa nambari mbili nyuma ya Mbelgiji Thibaut Courtois msimu ujao wa 2019-2020 wakati huu kipa nambari moja Keylor Navas anaonekana yumo mbioni kuondoka.

Hofu kuhusu ‘kuiva’ kwa chipukizi Luca, 21, kutwikwa majukumu ya kipa nambari mbili baada ya kuwa michumani mara mbili pekee kwenye Ligi Kuu ya Uhispania imezingira suala hili.

Gazeti la Marca nchini Uhispania sasa linadai kwamba viongozi wa Real Madrid wangependelea kuona Andriy Lunin, 20, ambaye yuko katika klabu ya Leganes kwa mkopo, akiwa kipa nambari mbili nyuma ya Courtois.

Zidane aliondoka Madrid kwa ghafla mwisho wa msimu 2017-2018 kabla ya kuajiriwa tena Machi mwaka huu na inasemekana yuko tayari kuchukua hatua kama ya kwanza asiposikizwa