Zifahamu faida za hiliki

Zifahamu faida za hiliki

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

WAPISHI wengi wanapenda kutumia hiliki kwa kuwa inaongeza ladha na harufu nzuri kwenye vyakula.

Pamoja na kuchochea harufu nzuri, pia ina virutubisho vingi ikiwa ni pamoja na Vitamini A na C, madini ya calcium, potassium, sodium, copper, zinc na magnesium.

Pia hilliki ina wanga gramu 68, protini 11 na nyuzinyuzi gramu mbili.

Pia inaipa figo uwezo wa kuondoa taka mwilini na kusaidia kuweka sawa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula tumboni.

Hiliki pia inasaidia kuondoa hali ya kiungulia na gesi tumboni na tatizo la kukosa choo.

Jinsi unavyoweza kuitumia hiliki

Saga hiliki kisha tumia unga wake kijiko kimoja cha chakula katika maji moto yaliyo katika kikombe cha chai.

Kunywa kila siku na bila shaka baada ya muda wa wiki mbili utaona matokeo mazuri katika mwili wako.

Pia ina uwezo mkubwa wa kuboresha mishipa ya damu kwenye moyo na hivyo kuulinda dhidi ya magonjwa na matatizo mbalimbali ya moyo.

Inaondoa maradhi ya kinywa – hasa kinachotoa harufu mbaya – na kutibu vidonda vya mdomoni. Unachotakiwa kufanya ni kuchukua unga wa hiliki uliochanganywa na maji fufutende kisha usukutue mdomoni kila siku asubuhi na jioni kwa kipindi cha wiki tatu.

Tumia kijiko kimoja cha unga wa hiliki katika uji usio mzito katika kikombe cha chai kila siku muda wa wiki mbili.

Hiliki pia inasaidia kukinga saratani na shinikizo la damu iwapo utatumia kwa kuzingatia maelekezo kutoka kwa wataalamu wa afya.

Pia ina uwezo wa kuondoa tatizo la pumu katika hatua za awali na inapochanganywa na mdalasini husaidia kupunguza maumivu ya koo.

You can share this post!

MIAKA 40: Museveni ashinda urais kwa mara ya sita mfululizo

Mchakato wa kumsaka mrithi wa Maraga kuanza Jumatatu