Ziwa Naivasha hatarini

Ziwa Naivasha hatarini

NA RICHARD MUNGUTI

WATAFITI wametoa tahadhari kwamba uwepo wa madini ya sumu katika Ziwa Naivasha inahatarisha maisha ya samaki pamoja na wanyama wengine wanaoishi majini.

Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo, athari za madini hayo ni kwamba maisha ya wanyama wa majini yamo hatarini.

Imesemekana kwenye ripoti hiyo kwamba wizara ya afya inayohusika na afya ya binadamu haijatoa ufafanuzi zaidi kuhusu madini hayo ya sumu katika maji ya matumizi.

Imebainika kuwa samaki aina mbali mbali wameendelea kutokomea polepole.

Wataalam wamesema kiwango cha pH katika maji hayo ya Ziwa Naivasha ni kati ya 6 na 8.

Uchafuzi wa mazingira umechangia pakubwa katika ongezeko la madini ya sumu katika ziwa hilo.

Wataalam hao wamesema kuwa mmomonyoko wa udongo kutokana na shughuli za kilimo mashariki mwa ziwa hilo umechangia katika uchafuzi wa ziwa hilo.

Pia dawa na kemikali zinazotumika katika kilimo zimeongeza kuhatarisha zaidi mazingira ya ziwa hilo.

Pamoja na hayo, shughuli za kitalii hazijaachwa nyuma katika uchafuzi wa ziwa hilo lililo na maji safi.

  • Tags

You can share this post!

Mshukiwa wa wizi wa vyuma vilivyoibwa kutoka Industrial...

‘Tatizo la vijana kukosa kazi lastahili...

T L