Bambika

Zuchu sasa amtema Diamond, aahidi kumakinikia kazi WCB

February 24th, 2024 1 min read

NA FRIDAH OKACHI

MWANAMUZIKI Zuhura Othman almaarufu Zuchu ametangaza rasmi kuvunjika kwa mahusiano yake mpenzi wake Diamond Platnumz.

Katika ukurasa wake wa Instagram mnamo Ijumaa, mwanamuziki huyo alikiri kwa muda mrefu amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na bosi huyo wa WCB.

“Habari familia, nahitaji kuweka sawa dhamiri yangu. Kuanzia leo hii mimi na Nasibu (Diamond) hatuko pamoja,”  alianza Zuchu.

Mwanamuziki Zuchu. PICHA | HISANI

Akaongeza: “Najua hili limekuwa jambo letu lakini ni ngumu kumuacha mtu unaempenda.  Naomba kwa Mungu hili liwe la mwisho na nianze maisha mapya. Mapenzi ni heshima na kwa bahati mbaya sana, hilo lilikosekana kwetu.”

Hata hivyo kwenye ujumbe huo, malkia huyo wa sauti ya ninga aliweka wazi kuwa ataendelea kufanya kazi–tena kwa ushirikiano mkubwa–na kikosi cha WCB Wasafi.

Soma Pia: Zuchu adai Diamond ndiye mwanamume wa kwanza kumpa burudani chumbani

Alisema atatii makubaliano katika mkataba aliotia saini na lebo ya WCB.

Pia kwenye chapisha hilo refu, Zuchu alilalamikia mahusiano yako kutokuwa sawa.

“Tumeishi vizuri lakini nadhani hii sio riziki… Nimejifunza kusema hapana kwa kila kitu kisichonipa furaha. Ama baada ya kusema haya ninaanza ukurasa mpya wenye furaha, uhuru na amani… Kwa sasa kazi iendelee na mimi niko single,” akasema.

Mnamo Alhamisi soshiolaiti Zari Hassan, alipakia video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa amemshika mkono mwanamuziki Diamond ambaye kabla ya kutemana, walijaliwa watoto wawili.

Hata hivyo bosi wa WCB alikuwa wa kwanza kwenye ukurasa wa instagram akimtambulisha kuwa dadake.

“Mimi na dada @zarithebosslady,” aliandika Diamond.

Mnamo Januari 2024, mwanamuziki huyo alikuwa wa kwanza kutangaza kwamba mapenzi hayakuwa yakimwendea sawa.

Alisema yuko singo lakini baada ya saa kadha, alibadilisha mawazo.

“Kuanzia leo ningependa niwatangazie rasmi kuwa I AM SINGLE, sichumbii wala sina mahusiano na mwanamke yeyote,” alisema Diamond kabla ya kubadilisha mawazo.