Habari za Kitaifa

FKE yapata Rais wa kwanza mwanamke

May 30th, 2024 1 min read

NA JAEL MAUNDA

MSOMI Dkt Gilda Odera ndiye mwanamke wa kwanza kuwa rais wa Shirikisho la Waajiri Nchini Kenya (FKE) baada ya kuchaguliwa katika makala ya 65 ya Mkutano Mkuu wa Mwaka mnamo Jumatano.

Dkt Odera alichaguliwa katika uchaguzi uliofanyika katika hoteli ya JW Mariott jijini Nairobi Jumatano.

Anachukua usukani kutoka kwa Dkt Habil Olaka aliyehudumu kwa kipindi cha miaka miwili.

 

Rais mpya ajaye wa Shirikisho la Waajiri Nchini (FKE) Dkt Gilda Odera, mkurugenzi mtendaji Jacqueline Mugo na Rais wa FKE anayeondoka Habil Olaka wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa FKE–makala ya 65–katika JW Marriott, Nairobi mnamo Mei 29, 2024. PICHA | BILLY OGADA

Kabla ya kuchaguliwa kuongoza shirikisho hilo, Dkt Odera alikuwa naibu wa kwanza wa rais katika FKE  kwa miaka miwili iliyopita.

“Ninaahidi kushirikiana na serikali iliyoko mamlakani kwa nia moja tu ya kutimiza malengo ya FKE,” akasema Dkt Odera.

Naibu wake wa kwanza katika FKE ni Bw Mike Macharia naye Bw Laurence Okelo alichaguliwa naibu wa pili.