Michezo

Manchester United ilivyoporomoka hadi viwango wa kihistoria Ligi Kuu

May 21st, 2024 2 min read

MANCHESTER, UINGEREZA

TIMU ya Manchester United iliporomoka hadi nafasi ya nane katika msimamo wa mwisho wa 2023/24 wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ambao ulikamilika Jumapili.

Katika historia ya United, hawajawahi kumaliza chini ya nafasi ya saba EPL.

Ilipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Brighton ugenini siku ya mwisho ya ligi.

Mabao hayo yalitiwa kimiani na Diogo Dalot na Rasmus Hojlund dakika ya 73 na 89.

Mara ya mwisho walimaliza nafasi ya saba walikuwa chini ya kocha David Moyes.

United sasa wamekamilisha kampeni wakiwa na tofauti mbaya ya mabao kwa mara ya kwanza tangu timu ya Sir Alex Ferguson ya 1989-90, ikimaliza kwa -1, tangu ilipoanzishwa mwaka 1992.

Mara ya mwisho walimaliza chini ya nafasi ya saba ilikuwa mwaka 2014, ikiwa chini ya David Moyes msimu mmoja tu baada ya Sir Alex Ferguson kustaafu.

United sasa sasa lazima ielekeze mawazo yao kwenye fainali ijayo ya Kombe la FA dhidi ya mabingwa wa EPL Manchester City, ambao waliipiku Arsenal kwenye taji la EPL kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya West Ham United.

Kwa upande mwingine, Aston Villa inamaliza nafasi ya nne na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 41 chini ya meneja Unai Emery.

Walimaliza nafasi ya nne nyuma ya Manchester City, Arsenal na Liverpool ambao walimaliza nafasi ya kwanza, pili na tatu mtawalia.

Villa haijafuzu kwa mashindano hayo tangu 1983, baada ya kushinda Ligi ya Mabingwa, au Kombe la Uropa, mnamo 1982.

Hii ndio nafasi bora walimaza tangia 2010. Villa wamemaliza tu katika nafasi nne za juu kwenye Ligi ya Premia mara mbili katika historia yao, mara ya mwisho ilikuwa 1996.

Sasa bila shaka wana changamoto kubwa zaidi katika utawala wa Emery, huku wakikabiliana na kukaribisha timu kubwa zaidi za Ulaya nyumbani Villa Park.

Licha ya kuanza vibaya kwa msimu, Chelsea ilifanikiwa kumaliza nafasi ya sita na kupata nafasi ya kucheza soka la Ulaya.

The Blues waliwazaba Bournemouth uwanjani Stamford Bridge Jumapili 2-1 na hivyo kuhitimisha kampeni ya kwanza ya Mauricio Pochettino kuinoa timu hiyo.

Moises Caicedo aliifungia Chelsea mbele katika kipindi cha kwanza. Muda mfupi baada ya mapumziko, Raheem Sterling alifunga bao la pili.

Chelsea walifanikiwa kushikilia na kujihakikishia nafasi ya sita, lakini bado haijafahamika iwapo watacheza Ligi ya Europa au Ligi ya Conference msimu ujao.

Ingawa wenyeji wa London Magharibi hawako, bila shaka, katika fainali ya Kombe la FA, pambano hilo bado ni muhimu sana kwao.

Manchester United na Manchester City zitamenyana Wembley Jumapili, Mei 25, huku Red Devils wakiwa na hamu ya kulipiza kisasi kwa wapinzani wao kwa fedheha ya mwaka jana.

Wanaweza wakacheza Europa msimu ujao – ikiwa City itaipiga United katika fainali ya Kombe la FA.

Wakati uo huo, huenda Newcastle ambao walimaliza nafasi ya saba EPL, wakacheza Ligi ya Conference iwapo City watapata ushindi FA lakini watakosa kucheza Ligi ya Europa ikiwa United watatwaa ubingwa.