Habari Mseto

Meneja ashtakiwa kujishindia kazi akitumia vyeti feki na kumumunya mshahara wa Sh1.4m

April 3rd, 2024 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA meneja mkuu wa masuala ya kifedha katika shirika la kusambaza umeme la Rural Electrification and Renewable Energy (Rerec) Noach Okech Oluoch almaarufu Noah Oketch Oluoch ameshtakiwa kujishindia kazi hiyo akitumia cheti feki cha degree kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, na kumumunya mishahara ya Sh1.4 milioni kinyume cha sheria.

Hakimu mkuu katika mahakama ya kuamua kesi za ufisadi Milimani Bw Thomas Nzioki alifahamishwa na kiongozi wa mashtaka Caroline Kimiri kwamba Oluoch alighushi cheti cha digrii ya uzamifu katika masuala ya biashara na fedha kutoka Chuo hicho.

Bi Kimiri alisema mshtakiwa aliajiriwa kazi ya Umeneja na Msimamizi wa Teknolojia katika shirika la Rerec kwa sababu ya kuhitimu kwake.

Hata hivyo, alikana mashtaka matatu na kuachiliwa kwa dhamana ya pesa tasilimu Sh500,000. Kesi itatajwa Aprili 17, 2024 kutengewa siku ya kusikizwa na maagizo mengine zaidi.