Afya na Jamii

Ninaendesha sana, sijui sababu ni gani

June 3rd, 2024 1 min read

Mpendwa Daktari,

Nimekuwa nikiendesha kila wakati. Nini kinachosababisha hali hii?

Winfred, Mombasa

Mpendwa Winfred,

Kuendesha kunakosababshwa na maambukizi ya virusi vya; rotavirus, ambavyo huwakumba sana watoto wadogo, na norovirus, ambavyo huwakumba watu wakomavu na watoto walio katika umri wa kwenda shuleni.

Pia kuna adenovirus ambavyo huwakumba watu wa umri wote.

Ishara kamili za kuendesha

>> Kutokwa na kinyesi cha majimaji. Kinyesi hiki chaweza kuwa cha rangi yoyote huku rangi nyekundu ikiashiria kuwa matumbo yanavuja.

>> Maumivu makali ya tumbo. Huenda ni dalili ya maradhi mabaya.

>> Homa. Hali hii sio kawaida kuambatana na maradhi haya na hivyo unashauriwa kupata matibabu kila unaposhuhudia dalili hii.

Kukaukiwa na maji mwilini kunakojitokeza kwa ishara kama vile:

  • Kwa watu wakomavu, kukauka mdomo na kuhisi kiu kila mara.
  • Kwa wazee ngozi huonekana nyepesi huku mgonjwa akihisi usingizi kila mara na hata kuchanganyikiwa.
  • Kwa watoto wadogo, ishara kuu huwa macho kuzama usoni, kukauka mdomo na kukojoa kila mara kuliko kawaida. Watoto wengi hukumbwa na usingizi kila mara na hata kukataa kula.

Wakati upi wa kutafuta matibabu?

Unashauriwa kutafuta matibabu unaposhuhudia ishara zifuatazo:

  • Iwapo kuendesha kunaambatana na homa kali, maumivu makali ya tumbo au kukaukiwa na maji ambako hakuwezi kabiliwa na matumizi ya vyakula vya majimaji.
  • Iwapo kinyesi hiki kitaambatana na damu
  • Iwapo mgonjwa anaonekana kushikwa na usingizi kila mara na anaonesha tabia zisizo za kawaida.
  • Kutapikana kushindwa kula au kunywa
  • Iwapo mhusika ni mzee au ana matatizo ya kiafya kama vile kisukari, matatizo ya moyo, figo, maini au ana virusi kwa HIV.