Makala

Ex wa Alikiba afunguka kuhusu mahusiano haramu akiwa kwenye ndoa

April 8th, 2024 2 min read

NA SINDA MATIKO

MTANGAZAJI maarufu wa Wasafi FM, Diva The Bawse amemwaga ubuyu kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na staa wa bongo flava Alikiba.
Ni uhusiano ambao pia, unamhusu aliyekuwa mke wa Alikiba Mkenya Amina Khaleef ambaye alitangaza kuachana naye akimshutumu kwa kuitelekeza familia yake, kumwonyesha dharau na michepuko.

Akitoa za ndani Diva, anasema wengi wasichokijua ni kwamba yeye na Alikiba walikuwa ni wapenzi kwa miaka mingi sana na waliweza kuyaweka mahusiano yao siri nje ya macho ya umma. “Kabla Ali hajaoa, nilikuwa naye, kabla ya wanawake wote hao nilikuwepo mimi na yeye na yalikuwa ni mapenzi chini ya maji sana. Sikuwa mchepuko. A

lipooa nilikuwa pembeni. Kukatangazwa kuna utengano wameachana (yeye na Amina) hapo ndipo tukafufua tena mahusiano yetu,” Diva kafunguka.

Hata hivyo, Diva anasema baadaye alikuja kugundua kuwa Alikiba hakuwa ametengana na Amina kama ilivyokuwa imetangazwa na hapo akaamua kumdampu.

“Niliposkia kwamba hajamtaliki yule dada, nikajiengua na kujiweka pembeni tena. Nilimwambia Ali hatuwezi kufanya hichi kitu. Na hii ndio taabu ambayo hunitokea, kila ninapomwambia mtu siyataki mahusiano haya tena, lazima huyo mtu ataniponda.

Kwanza atanibembeleza baadaye ataanza kuniponda baadaye atarudi tena na ndio maana mwisho wa penzi letu haukuwa mzuri,” Diva kaongeza.
Amina aliwasilisha ombi la  talaka 2022 kwenye mahakama ya kadhi mjini Mombasa na kuiambia mahakama hiyo kwamba alikuwa ameshindwa kuendelea na ndoa hiyo kutokana na Alikiba kuitelekeza na kuishi kuwa na michepuko.

Kuna kipindi jina la Diva liliwahi kuhusishwa na tetesi hizo za kuwa mchepuko wa Ali jambo analolipinga kabisa akisisitiza hakuwahi kuwa mpango wa kando wa Ali wakati akiwa kwenye ndoa na Amina.

“Sikuwa mpango wa kando. Na sababu ya Ali kutonioa ni kwa sababu sikuwa tayari kuolewa. Kwa kipindi kile, sikuwa tayari kuwa mke, nilikuwa mdogo. Ali alikuwa tayari kunioa ila sikuwa tayari,” anasema Diva.

Toka waachane na Diva kuingia kwenye mahusiano mengine, anasema hisia za mapenzi kwa Alikiba zilimwishia kabisa na kwa sasa anamwangalia tu kwenye ango ya mwanamuziki mzuri na wala si vinginevyo.

Hata hivyo, anasisitiza kuwa penzi lao lilipodumu, waliishia kuwa na bondi kubwa mno hata kama ‘hatukukilikiana’.

“Mimi na Ali tulikuwa na bondi kubwa mono licha ya kilichotokea, tulipendana sana na nafikiri ndio sababu mwisho wa penzi letu ulikuwa mbaya sana. Mambo hayakuingiana, lakini kuna vitu vizuri vilikuwepo vingi kuliko vitu vibaya.”