Makala

MAPISHI: Pasta na meatballs zenye cheese

May 15th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MUDA wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa kupika: Dakika 30

Walaji: 2

Vinavyohitajika

  • 250g/ nusu paketi ya tambi
  • Kilo ½ ya meatballs
  • Nyanya 1 kubwa
  • Kitunguu 1
  • Kijiko 1 cha kitunguu saumu
  • Kijiko 1 cha tangawizi
  • Kikombe 1 nyanya ya kopo
  • Vijiko 2 vya mafuta ya mzaituni
  • Kikombe 1 maji
  • ½ kikombe mozzarella cheese
  • Majani ya giligilani

Maelekezo

Weka nyanya na kitunguu kwenye blenda kutengeneza rojo; twanga kitunguu saumu na tangawizi kwa ajili ya sosi, weka kando.

Katakata mozzarella cheese vipande vidogovidogo vya mraba, katakata pilipili na majani ya giligilani vipande vidogovidogo.

Meatballs. Picha/ Margaret Maina

Kwenye sufuria katika moto wa juu kiasi, chemsha mafuta kiasi cha vijiko viwili. Ongeza meatballs. Kaanga kwa dakika mbili au mpaka iwe ya kahawia kwa nje ila isiive kabisa.

Hamisha nyama kwenye sahani.

Chemsha tambi ukifuata maelezo yaliyoko kwenye paketi. Chuja maji, weka pembeni.

Kwenye sufuria uliyotumia kupika nyama, rudisha kwenye moto. Ongeza vijiko viwili vya mafuta, yakichemka ongeza kitunguu saumu na tangawizi pika mpaka viive.

Pasta na meatballs. Picha/ Margaret Maina

Ongeza rojo ya nyanya na nyanya ya kopo, koroga vizuri.

Pika mpaka nyanya ziive vizuri.

Ongeza kikombe kimoja cha maji, acha yachemke mpaka sosi ianze kutokota.

Ongeza nyama, pika kwa dakika tano au mpaka iive vizuri. Kuwa mwangalifu isiive sana kwa sababu cheese kuanza kuchuruzika kwa nje.

Ongeza tambi zilizochemka, pika kwa dakika zingine mbili.

Weka majani ya giligilani. Toa kwenye moto.

Pakua chakula kiliwe kikiwa bado moto