Michezo

Roho mkononi Gor ikimenyana na USM Alger

August 29th, 2018 Kusoma ni dakika: 2

Na Geoffrey Anene

MASHABIKI wa Gor Mahia wamemgeukia Mungu kuona timu yao ikisonga mbele kwenye Kombe la Mashirikisho la Afrika mwaka 2018.

Gor ya kocha Dylan Kerr itamenyana na wenyeji USM Alger katika mechi yake ya mwisho ya Kundi D hapo Jumatano saa kumi jioni.

“Sisi sote tunaombea timu yetu (Gor). Mungu awe upande wetu,” shabiki Damianus Nyasoro amesema.

Safe Smartbomb, “Mungu hatawaacha wakati huu mnamuhitaji hata zaidi.”

Robert Ochieng, “Kila la kheri mabingwa wetu. Tuna imani nanyi. Jiamini uwanjani na nendeni mfanya kazi nzuri. Kwa Baraka za Mungu tutafaulu.”

“Mungu awe nanyi,” Chris Ouma Otieno anasema. Haya ni baadhi tu ya maoni ya mashabiki wa Gor inapojiandaa kuteremka uwanjani kusakata mechi hii ilio na umuhimu mkubwa kuamua kama inasalia mashindanoni ama la. Gor na USM Alger zinashikilia nafasi mbili za kwanza kwa alama nane kila moja.

Zote ziko katika nafasi nzuri ya kutinga robo-fainali na pia katika hatari ya kufungiwa nje ikiwa nambari tatu Rayon Sports ya Rwanda, ambayo ina alama sita, itapiga Young Africans nayo Gor ama USM Alger ipoteze. Gor na USM Alger zitaingia robo-fainali ikiwa Rayon itapoteza jijini Kigali ama kutoka sare. Zitafuzu pia ikiwa zitatoka sare nayo Rayon ishinde Young Africans pembemba.

Timu zitakazomaliza katika nafasi mbili za kwanza kwenye kundi hili zitaingia mduara wa nane-bora na kutia mfukoni Sh35, 269,500.

Mechi za robo-fainali zimeratibiwa kusakatwa kati ya Septemba 14 na Septemba 23. Droo ya robo-fainali itafanywa Septemba 3.

Vikosi:

USM Alger

Makipa – Mohamed Zemmamouche na Mourad Berrefane;

Mabeki – Mohamed Rabie Meftah, Redouane Cherifi, Abderrahim Hamra, Farouk Chafai, Elice Doris Nyeck (Mexes), Mokhtar Benmoussa, Mehdi Benchikhoune;

Viungo – Oussama Chita, Hamza Koudri, Amir Sayoud, Raouf Benguit;

Washambuliaji – Prince Ibara, Abderrahmane Meziane, Faouzi Yaya, Oualid Ardji, Aymen Mahious; Kocha Mkuu – Thierry Froger (Ufaransa)

Gor Mahia

Bonface Oluoch, Fredrick Odhiambo, Haron Shakava, Joash Onyango, Wesley Onguso, Karim Nzigyimana, Ernest Wendo, Humphrey Mieno, Bernard Ondiek, Lawrence Juma, Francis Kahata, George Odhiambo, Samuel Onyango, Jacques Tuyisenge, Francis Mustapha, Charles Momanyi na Philemon Otieno; Kocha Mkuu – Dylan Kerr (Uingereza)