• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:25 PM
OKTOBA 10: Wakili aelezea jinsi ya kusherehekea Moi Dei

OKTOBA 10: Wakili aelezea jinsi ya kusherehekea Moi Dei

Na PAULINE ONGAJI

IWAPO unapanga kukutana na marafiki kwa kinywaji huku ukijiandaa baadaye kujinyosha kwenye blanketi na kufurahia usingizi, pasi wasiwasi wa kurauka kwenda kazini Jumatano, basi kuna mtu mmoja wa kushukuru.

Bw Gragory Oriaro Nyauchi, wakili ambaye alijitolea kuwasilisha kesi mahakamani kupigania kurejeshwa kwa sikukuu hii ya kitaifa ya Moi Dei ambayo ilifutiliwa mbali kufuatia kurasmishwa kwa Katiba mpya ya 2010.

Wakili Oriaro aliwasilisha kesi hii mahakamani kwa mara ya kwanza mwezi Mei 2017  kabla ya Jaji wa Mahakama Kuu George Odunga kutoa uamuzi mwezi Novemba mwaka 2017 kurejesha sikukuu hii.

“Naamua kwamba Oktoba itasalia kuwa sikukuu ila tu endapo Bunge litabadilisha sheria kuhusiana na sikukuu, au endapo waziri atabadilisha siku hii ili kuadhimisha sikukuu ingine,” alisema.

Hata hivyo kumekuwa na sintofahamu kuhusiana na maadhimisho ya sikukuu hii iliyonuiwa kuwa kwa heshima ya Rais Mstaafu Daniel Moi.

Kwanza kabisa kama mtetezi wa kurejeshwa kwa sikukuu hii tutatulie sintofahamu hii na upendekeze jinsi siku hii inapaswa inapaswa kuadhimishwa.

Bila shaka! Kwanza kabisa siku hii inapaswa kuwa fursa kwa watu wengi kukaa nyumbani na familia zao. Pia watu wanapaswa kutumia wakati huu kuwazia masuala yanayolikumba taifa hili kama vile gharama ya juu ya maisha, ukabila, suitafahamu kuhusiana na katiba iliyopo.

Pia ni wakati wa kutafakari kuhusu tatizo la kukosa upinzani nchini, shida ambayo siwezi sema kwamba imetokana na salamu baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga, bali kutokuwepo kwa kipengee kuhusiana na suala hili  kwenye katiba ya sasa.

Suala la maadhimisho ya sikukuu sio muhimu kwa watu wengi. Nini kilichokupa mostisha wa kuwasilisha kesi hii?

Nilitaka kudhihirisha kwamba sio raia pekee wanapaswa kuzingatia sheria. Hata serikali ina jukumu la kufanya hivyo ambapo kwa kufutilia mbali sukukuu hii basi sheria ilikiukwa. Hili lilipaswa kuwa funzo.

Kadhalika niliona kwamba sio Wakenya wengi wanaopata siku za mapumziko kazini, kumaanisha kwamba wao hutegemea sikukuu na hivyo haikuwa haki kuwanyima siku hii. Pia hii imetoa ishara kali na nina uhakika kwamba wengi watanishukuru baada ya kupata fursa ya kupumzika hapo kesho.

Bila shaka wafanyakazi wengi wamefurahia kwamba hii leo wako nyumbani. Je kuna baadhi ambao wamewasiliana nawe wakitaka kukushukuru kwa kufanikisha haya?

Kirasmi la, lakini kuna baadhi ya marafiki ambao wameahidi kuninunulia vinywaji leo jioni.

Na upande wa waajiri, kuna wale ambao wamejaribu kuwasiliana nawe ili kukusuta?

Kama tujuavyo, katika biashara nyingi sikukuu inamaanisha kwamba hakuna pesa zitakazoundwa kumaanisha kwamba lazima kuna baadhi ambao wamekasirika ila hawajawasiliana rasmi nami kunijuza kuhusu lalama zao.

You can share this post!

Jacque Maribe atumwa Mathari kupimwa akili

Ajabu ya mwili kuhifadhiwa mochari kwa miaka 15 Machakos

adminleo