• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Kipchoge na Chepkoech watawazwa wanamichezo bora Septemba na Agosti

Kipchoge na Chepkoech watawazwa wanamichezo bora Septemba na Agosti

Na GEOFFREY ANENE

WASHIKILIZI wa rekodi za dunia Beatrice Chepkoech na Eliud Kipchoge wameibuka washindi wa Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa mwezi Agosti na Septemba ya Chama cha Waandishi wa Michezo (SJAK), mtwalia.

Katika hafla ya kuwatuza ilioandaliwa Oktoba 16, Chepkoech alinyakua taji la Agosti kutokana na rekodi ya dunia ya dakika 8:44.32 aliyoweka katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji kwenye duru ya Monaco ya Riadha za Diamond League mnamo Julai 20, 2018.

Alivunja rekodi ya ya dakika 8:52.78 ambayo Mbahraini Ruth Jebet aliweka katika duru ya Paris ya Diamond League nchini Ufaransa mwaka 2016.

Mfalme wa mbio za kilomita 42, Kipchoge alitawazwa mshindi wa tuzo hiyo wa mwezi Septemba kufuatia ushindi wake wa Berlin Marathon nchini Ujerumani mnamo Septemba 16, 2018. Kipchoge alitimka umbali huo mjini Berlin kwa saa 2:01:39 akifuta rekodi ya Dennis Kimetto ya saa 2:02:57 iliyokuwa imara tangu mwaka 2014.

Wakimbiaji hawa nyota walizawadiwa kombe, Sh100,000 na runinga ya kidigitali ya StarTimes ya inchi 43 kila mmoja.

Washindi wa matuzo ya mwezi ya SJAK (2018):

Septemba – Eliud Kipchoge (riadha)

Agosti – Beatrice Chepkoech (riadha)

Julai –

Juni – Manvir Baryan (mbio za magari)

Mei – Judy Waguthii (bondia)

Aprili – Wycliffe Kinyamal (riadha)

Machi – Geoffrey Kamworor (riadha)

Februari – Felmas Adhiambo (mpira wa vikapu)

Januari – Cynthia Onyango (mpira wa magongo)

You can share this post!

Canada nayo pia yahalalisha matumizi ya bangi

Machifu kupokea mafunzo ya kijeshi

adminleo