Akwana kusaidia kuinoa KCB ligini
Na JOHN ASHIHUNDU
Aliyekuwa beki matata wa klabu ya AFC Leopards na Harambee Stars, Ezekiel Akwana amepewa jukumu la kuwa naibu kocha wa timu ya Kenya Commercial Bank (KCB) ambayo itashiriki Ligi Kuu ya Kenya (KPL) msimu ujao.
Kocha huyo wa zamani wa Sofapaka FC, AFC Leopards na Nakuru All Stars pamoja na Elvis Ayany watakuwa manainu wa Franl Obuna.
Akwani aliagana na Nakuru All Stars miezi kadhaa iliyopita na amekuwa akisaidia vijana mitaani kunoa vipaji vyao.
KBC wamerejea katika Ligi Kuu ya Kenya (KPL) baada ya kuteremshwa miaka mitatu iliyopita.
Kocha mkuu, Ouna anaendelea kuzungmza na wachezaji kadhaa kwa lengo la kuiongezea timu hiyo nguvu kwa ajili ya msimu wa 2018/19 utakaoanza Desemba 8.
Ouna alikuwa na Wazito msimu uliopita, lakini ameamua kuondoka baada ya klabu hiyo kuteremshwa ngazi hadi daraja la Supa Ligi.
Wazito walimaliza katika nafasi ya 17 jedwalini kwa pointi 31, nane Zaidi kuliko Thika United waliomaliza mkiani.
Pamoja na Western Stima, KCB imepanda ngazi kunogesha kipute cha msimu ujao baada ya kumaliza katika nafasi mbili za kwanza.
Timu ya tatu kupanda itaamuliwa baada ya mikondo miwili ya mchujo kati ya Nakumatt na Ushuru FC.