Nilaumiwe kwa kadi nyekundu ya Hugo Lloris – Pochettino
Na CECIL ODONGO
KOCHA wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino amekataa kumlaumu mnyakaji wa timu hiyo Hugo Lloris kutokana na sare ya 2-2 waliyosajili dhidi ya PSV ya Ufaransa katika mechi za kuwania klabu bingwa barani Afrika Jumatano Oktoba 24 usiku.
Mabao ya Harry Kane na Lucas Moira yaliwaweka Spurs kifua mbele baada ya Hirving Rodrigo Lozano kuwapa uongozini mibabe hao wa soka ya Ufaransa.
Hata hivyo kitumbua cha vijana wa kocha Mauricio Pochettino kiliingia mchanga Lloris alipotimuliwa uwanjani dakika ya 79 kwa kadi nyekundu na PSV wakatumia idadi yao wengi uwanjani kuwahangaisha Spurs na hatimaye kufunga bao la kusawazisha kupitia Luuk de Jong.
“Sitamlaumu mchezaji yeyote. Iwapo mtu ana nia ya kumlaumu mchezaji basi anilaumu mimi kwa sababu mimi ndiye nilitwikwa majukumu ya kuongoza timu. Hatukushinda,” akasema mkufunzi huyo raia wa Italia.
Vile vile alitetea wachezaji wake akisema walisakata soka ya kuridhisha ila wakati mwingine huwa vigumu kupata ushindi licha ya kujituma na kumiliki asilimia kubwa ya mchezo.
Katika mechi nyingine za Jumatano Oktoba 24 usiku, Dotrmond waliwapa aibu ya mwaka Atletico Madrid kwa kuwacharaza 4-0, PSG ya Ufaransa ikaagana sare ya 2-2 na Napoli, Lverpool wakawafunga Red Star Belgrade 4-0 nayo Galatasary ya Uturuki zikaumiza nyasi bure kwa sare tasa.
Barcelona ya Uhispania ilisagasa Inter Milan ya Italia 2-0 huku wakijitayarisha kuvaana na mahasimu wao wakuu katika LaLiga, Real Madrid.
FC Porto ya Ureno ilihitimisha mechi za Jumatano kwa kuwabamiza Locomotiv Moscow 3-0 ugenini.