Afya na Jamii

Kinachosababisha chunusi sehemu inayozingira uke

January 22nd, 2024 Kusoma ni dakika: 1

NA PAULINE ONGAJI

Wakati mmoja maishani, huenda kila mwanamke akakumbwa na tatizo la chunusi katika sehemu inayozingira uke.

Ni suala linalowapa wengi wasiwasi, kiwango cha kuwakosesha starehe.

Kiini

Kuna mambo kadha wa kadha ambayo yaweza sababisha hali hii.

Kwa mfano, chunusi katika sehemu hii yaweza kuwa tokana na maambukizi ya ukuvu, bakteria au virusi.

Pia hali hii yaweza sababishwa na kuvimba na/au maambukizi katika vinyweleo vya vywele hasa baada ya kunyoa nywele za sehemu hii.

Aidha, baadhi ya watu hupata chunusi katika sehemu hii kutokana na mabadiliko ya kihomoni kabla, wakati au baada ya kushuhudia hedhi.

Pia, hii yaweza tokana na matatizo ya ngozi yanayoathiiri sehemu zingine za mwili na hivyo kuenea hadi katika sehemu hii. Kando na hayo, hii yaweza kuwa ishara ya mzio.

Ili kutambua kiini kamili cha hali hii unashauriwa kumuona daktari ili uchunguzi ufaao ufanywe na upate matibabu yanayohitajika.