Ukosefu wa maji salama tishio kwa lishe na usafi – ripoti
NA MWANGI MUIRURI
KAUNTI ya Murang’a imeshindwa kufanikisha malengo ya Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu lishe na usafi kutokana na ukosefu wa maji salama ya kunywa.
Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Murang’a Kusini, Kandara, Kiharu, Ithanga, Kakuzi na Kigumo, kwa mujibu wa Taasisi ya Utamaduni na Ekolojia (ICE).
Ripoti mpya iliyotolewa na ICE 2023, inaashiria kuwa, kutokana na kiwango cha chini cha maji ya mifereji, mtoto mmoja kwa kila watoto watano amedumaa kwa sababu ya lishe duni