Akili MaliMakala

Wakulima wahimizwa kujiundia chakula cha mifugo kukwepa bei ghali

Na SAMMY WAWERU August 19th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

WAKULIMA wa mifugo nchini wamehimizwa kukumbatia mbinu za kibunifu kujitengenezea chakula cha mifugo ili kukabiliana na gharama ya juu ya malisho ya madukani.

Kulingana na watafiti, mbinu ya kujiundia malisho itasaidia kupunguza gharama ya uzalishaji.

Wakulima, hata hivyo wanapaswa kuwa na kiini au chanzo Hali kadhalika, wanashauriwa kuwa na ufahamu bora wa jinsi ya kutengeneza lishe ya mifugo.

Bw Maurice Msanya, ambaye ni mtafiti na daktari wa mifugo, anahimiza wanaoendeleza ufugaji-biashara wa kufanya majaribio ya mifumo tofauti ya kuunda chakula cha mifugo ili kupata faida.

DktMaurice Msanya, mtaalamu wa mifugo kutoka Bimeda akihamasisha wafugaji jinsi ya kujiundia malisho kwenye kongamano Jijini Nairobi. PICHA|SAMMY WAWERU

“Na ndiyo sababu ninahimiza wafugaji kukumbatia mbinu ya kujitengenezea lishe ya mifugo kukabiliana na ughali uliopo wa bidhaa hii nchini,” Dkt Msanya akaambia Taifa Dijitali kupitia mahojiano ya kipekee.

Mtaalamu huyu ni Meneja wa Mauzo katika shirika la Bimeda.

Anasikitika kwamba gharama ya juu ya malisho hasa ya ng’ombe wa maziwa, ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wakulima nchini.

Mfugaji akionyesha chakula cha kuku alichosaga. PICHA|SAMMY WAWERU

Bei ya lishe ya mifugo imekuwa ikiongezeka kila kukicha hasa tangu mkurupuko wa maradhi ya Covid-19 kushuhudiwa nchini.

Licha ya ulimwengu kutangazwa kuwa huru dhidi ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya corona, bei la malighafi muhimu imekuwa ikiongezeka.

Malighafi yenye madini ya Protini, ndiyo yameathirika pakubwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa na kuku wakiendelea kuhangaika.

Kenya huagiza zaidi ya asilimia 80 ya malighafi kutoka nje ya nchi.

Kuku ni kati ya mifugo iliyoathirika kutokana na bei ghali ya chakula cha madukani. PICHA|SAMMY WAWERU

Kando na athari za janga la Covid-19, kodi na ushuru wa ziada (VAT) wa juu unaotozwa bidhaa kutoka nje ya nchi umechangia kuendelea kuongezeka kwa bei ya chakula cha mifugo cha madukani.

Mkulima akiwa na fomula, mifumo ya kujitengenezea malisho itamuokoa.

Imetafsiriwa na Kalume Kazungu