Habari za Kitaifa

Masengeli akata rufaa kupinga kutupwa jela miezi 6

Na SAM KIPLAGAT, BENSON MATHEKA September 18th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

KAIMU Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli amekata rufaa kupinga adhabu ya kifungo cha miezi sita jela baada ya kuhukumiwa na Mahakama Kuu akisema alihukumiwa bila kusikilizwa.

Bw Masengeli anasema kwamba hakuhitajika kufika binafsi kortini, na alituma Naibu Inspekta Jenerali Eliud Langat kumwakilisha.

“Kwamba uamuzi wa Mahakama Kuu  ulinihukumu bila kusikilizwa, na kukiuka kabisa haki yangu isiyoweza kupuuzwa ya kusikilizwa kwa haki kama inavyotolewa chini ya Kifungu cha 25 cha Katiba,” aliongeza.

Aidha anasema uamuzi wa Jaji Lawrence Mugambi huenda uliathiriwa na mambo mengine.

Bw Masengeli aliiomba mahakama hiyo kusikiliza rufaa yake kwa haraka, akisema Jaji wa Mahakama Kuu alimpa muda wa siku saba ambao unamalizika Septemba 20 na kufungwa jela kutafanya rufaa yake kutokuwa na maana.

Habari zaidi kufutia…