Mashujaa Dei 2024: Kwa njia ya picha
RAIS William Ruto, Jumapili, Oktoba 20, 2024 ameliongoza taifa kuadhimisha Mashujaa Dei mwaka huu.
Mashujaa Dei, ni siku ya kitaifa nchini Kenya, ambayo huadhimishwa kila mwezi Oktoba tarehe 20.
Aidha, ni Sikukuu ya umma kuwaheshimu na kuwatambua kwa pamoja wananchi waliochangia katika mapambano kupata uhuru wa Kenya au waliochangia kwa njia chanya kuboresha taifa baada ya uhuru.
Sherehe za Mashujaa mwaka huu, 2024 zinafanyika katika Gatuzi la Kwale, Uga wa Kwale.
Rais Ruto ameandamana na Naibu Rais mteule, Prof Kithure Kindiki aliyemlaki rasmi.
Kauli mbiu ya Mashujaa Dei 2024 ni ‘Boma yangu’, kwa Kiingereza ‘Affordable Housing’.
Ujenzi wa nyumba za bei nafuu, ni mojawapo ya sera za Dkt Ruto kupitia ajenda kuu ya BETA – Mabadiliko ya Kiuchumi ya Chini Juu.
Picha zifuatazo zinatoa taswira kamili ya jinsi hafla hiyo inayoendelea ilivyo: