Jiandaeni kwa wikendi ya mvua, wakazi wa maeneo haya washauriwa
WAKENYA katika maeneo mbalimbali nchini wameshauriwa kujiandaa kwa mvua katika muda wa siku tano zijazo, hasa wikendi.
Katika ushauri wa hali ya hewa wa siku tano kati ya Ijumaa, Novemba 8 na Jumanne, Novemba 12, Idara ya Hali ya Hewa ya Kenya iliwashauri wakazi wanaoishi karibu na Nyanda za Juu Mashariki na Magharibi mwa Bonde la Ufa, Bonde la Ziwa Viktoria, Bonde la Ufa, Nyanda za Juu Kusini-mashariki , Pwani, na Kaskazini-mashariki mwa Kenya kujiandaa kwa mvua katika baadhi ya maeneo.
Idara ilifichua kuwa mvua inatarajiwa kunyesha katika maeneo haya katika nusu ya kwanza ya kipindi cha utabiri kuanzia Novemba 8-Novemba 10.
Nusu ya pili ya kipindi cha utabiri kinachoendelea kati ya Jumatatu na Jumanne wiki ijayo huenda kukawa na jua na ukavu zaidi.
Katika baadhi ya maeneo, mvua itaanza kunyesha Ijumaa asubuhi na kuendelea hadi usiku. Kulingana na utabiri, mvua pia itanyesha hadi wikendi, kisha itaendelea hadi Jumatatu na Jumanne. Jijini Nairobi, mvua itanyesha Jumamosi usiku, huku idara ikisema Jumamosi asubuhi kutakiwa na joto.
Kaunti za Siaya, Kisumu, Homabay, Migori, Kisii, Nyamira, Trans Nzoia, Baringo, Uasin Gishu, Elgeyo-Marakwet, Nandi, Nakuru, Marsabit, Mandera, Narok, Kericho, Bomet, Kakamega, Vihiga, Bungoma, Busia, na Pokot Magharibi. zimeorodheshwa kama kunakotarajiwa mvua.
Wenyeji wanaoishi katika kaunti hizi walishauriwa wawe waangalifu kwani mvua itaambatana na ngurumo za hapa na pale.
Wakazi wa maeneo ya Kaskazini Mashariki ya kaunti za Turkana na Samburu pia wametahadharishwa kuhusu mvua. Nairobi pia iko kwenye orodha hiyo, sawa na Mombasa, Kilifi, Lamu, Kwale, Machakos, Makueni, na kaunti zingine.