NIPE USHAURI: Nataka gunge anisaidie kuchimba kisima ila asije kudai umiliki
MKE wangu ana kiu ya mahaba ajabu.
Katika kipindi cha hivi majuzi nimekuwa nikishindwa kumridhisha chumbani na nahofia kwamba atapata wa pembeni. Kuzuia hili, namtafuta kaka atakayenisaidia kumridhisha pasipo kutaka uhusiano naye.
Usifikirie suala la kuomba usaidizi katika nyanja hii kwani utapokonywa mkeo. Wewe zungumza na mkeo kuhusu hisia zako na ikiwezekana mkubaliane jinsi ya kuimarisha mahaba yenu ili nyote mridhike.
Nimegundua mke wangu anatafunwa na shamba boi, nifanyeje?
Nimeishi na mke wangu kwa miaka 15 na kujaliwa watoto wanne. Hatujawahi kuwa na tatizo katika ndoa yetu kwa muda huu wote. Hata hivyo, hivi majuzi kupitia kwa rafiki yangu, niligundua kuwa mke wangu amekuwa akitafunwa na shamba boi nikiwa kazini. Nimuulizeje?
Ikiwa huu ni ukweli basi huenda nyote mko katika hatari ya kuambukizwa maradhi ya zinaa. Fanya uchunguzi wa ziada na ukishapata ushahidi basi husisha mshauri wa ndoa katika mjadala mtakaokuwa nao.
Mke anatishia kuniacha kwa sababu ya ugumba, tafadhali nipe ushauri
Tumeishi kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka kumi. Hata hivyo, mimi na mke wangu hatujajaliwa kupata mtoto ambapo baada ya kwenda hospitalini iligundulika kuwa ni mimi niliyekuwa na tatizo. Sasa mke wangu anatishia kuniacha.
Vyema!
Wakati kama huu sio vyema kuelekezeana kidole cha lawama. Hapa mtahitaji usaidizi wa mshauri wa ndoa. Pia, mnaweza tafuta usaidizi wa kimatibabu kwani siku hizi kuna mbinu za kiteknolojia zinazosaidia wanandoa wanaokumbwa na matatizo ya kupata watoto kwa njia ya kawaida, kuwa wazazi.