Habari za Kitaifa

Habari za hivi punde: Gavana Barchok akamatwa na EACC

Na VITALIS KIMUTAI February 6th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

GAVANA wa Bomet Prof Hillary Barchok amekamatwa na maafisa wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) wanaochunguza madai ya ufisadi katika kaunti hiyo.

Maafisa hao wanafanya operesheni katika makazi na ofisi yake.

Hii ni sehemu ya uchunguzi unaoendelea kuhusu madai ya mgongano wa maslahi na wizi wa pesa za umma katika kaunti ya Bomet ambao gavana huyo anashukiwa kuhusika.

Msemaji wa EACC Eric Ngumbi amethibitisha.

Habari zaidi kufuata…