• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Zamalek kutua Nairobi kuvaana na Gor

Zamalek kutua Nairobi kuvaana na Gor

Na GEOFFREY ANENE

MIAMBA wa Misri, Zamalek wanatarajiwa kutua jijini Nairobi mapema Ijumaa (3.30am) kwa mechi ya soka ya Kombe la Mashirikisho la Afrika dhidi ya wafalme wa Kenya, Gor Mahia itakayosakatwa Februari 3, 2019.

Zamalek ilituma onyo kali kwa wenyeji Gor kwa kupapura Misr El-Makassa 4-1 kwenye Ligi Kuu ya Misri mnamo Januari 29 kabla ya kufunga safari ya Nairobi.

Itakuwa na kipindi chake cha kwanza cha mazoezi uwanjani Utalii Grounds hapo Februari 1 jioni halafu katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani mnamo Jumamosi jioni. Mabingwa mara 12 wa Misri watakabiliana na Gor katika mechi hii ya Kundi D hapo Februari 3 uwanjani Kasarani.

Mabingwa mara 17 wa Kenya, Gor, pia walipata motisha kubwa katika mechi yao ya mwisho kabla ya kukutana na Zamalek baada ya kuchapa SoNy Sugar 2-0 kwenye Ligi Kuu mnamo Januari 30.

Kutazama mechi katika uwanja wa Kasarani katika katika sehemu za kawaida za mashabiki ni Sh200, huku ile ya wageni mashuhuri ikilipishwa Sh500. Mechi hii ya mkondo wa kwanza itasimamiwa na raia kutoka Msumbiji Celso Armindo Alvacao (refa wa kupuliza kipenga), Arsenio Chadreque na Zacarias Horacio Baloi (marefa wa kunyanyua vibendera) na Zefanias Chijamela (afisa wa nne). Kamishan wa mechi atakuwa raia wa Sudan Mamoun Bushara Nasir naye Helly Zafinimanga kutoka Madagascar ni Mratibu Mkuu.

Ratiba ya mechi za makundi za Gor Mahia (2019):

Februari 3 – Gor Mahia na Zamalek (Nairobi)

Februari 13 – Petro de Luanda na Gor Mahia (Angola)

Februari 24 – Gor Mahia na Hussein Dey (Nairobi)

Machi 3 – Hussein Dey na Gor Mahia (Algeria)

Machi 10 – Zamalek na Gor Mahia (Misri)

Machi 17 – Gor Mahia na Petro de Luanda (Nairobi)

  • Tags

You can share this post!

Kalonzo ni msaliti, mkabila, mwoga na adui wa handisheki...

Kenya kusaka tiketi ya CHAN 2020 dhidi ya Burundi

adminleo