Dondoo

Shugamami aangua kilio kwa  kutorokwa na ‘Ben Ten’ wake

Na JANET KAVUNGA February 16th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SHUGAMAMI wa hapa, aliacha vidosho katika saluni moja vinywa wazi alipolalamika kuwa, alitorokwa na barobaro ambaye amekuwa akimhudumia kwa mwaka mmoja sasa.

Mama aliwapata vipusa saluni na katika hali ya kupiga soga akadai amekuwa mpweke kwa muda, baada ya Ben Ten wake kumhepa.

“ Huyo kijana alihepa kwa kuwa nilikuwa nampeleka mbio chumbani hata hakuwa akiamini naweza kufanya hivyo.

Hata baada ya kumlisha vizuri na kumpa hela hakuweza kuhimili nderemo zangu chumbani,” mama alisema huku vipusa wakimshangaa kwa vile alionekana kukerwa na hatua ya barobaro huyo.

Mmoja wa vipusa alimwambia hafai kuwa akiwania vijana wa rika ya watoto wake naye akawaambia waache kumezea mate wazee wenye hela.