BambikaMakala

Mrembo Lehmann ‘kuadhibiwa’ kuvuka mipaka ya kuonyesha mashabiki uchi mitandaoni

Na MWANDISHI WETU March 18th, 2025 Kusoma ni dakika: 2

HUENDA wadhibiti wa Instagram wakamzuia kisura Alisha Lehmann, 26, kupakia picha zaidi za uchi kwenye mtandao huo wa kijamii baada ya kukiuka kanuni na kuendeleza utovu wa maadili.

Demu huyo anayechumbiana na mwanasoka Douglas Luiz wa Juventus, alilazimika kufuta na kuhariri baadhi ya picha na video za kuzingua alizopakia Instagram wiki jana baada ya sehemu kubwa ya mashabiki wake zaidi ya milioni 17 kulalamika.

“Hizo ni picha chafu anazostahili kuonyesha Luiz pekee chumbani mwao. Vinginevyo, zinamsawiri kuwa mtovu wa nidhamu. Naomba aadhibiwe kwa kuzimwa kabisa mitandaoni,” akasema shabiki mmoja.

Awali, Alisha alikuwa ameandika: “Nimekuwa ‘nikiwaroga’ kwa sura pekee. Sasa nimeweka makalio, mapaja, maziwa na sehemu ya nyuma ya mgongo. Hapo vipi?”

Baada ya kuonywa dhidi ya kupakia picha za sampuli hiyo, amefichua mpango wa kuachana kabisa na masuala ya uanamitindo ili kumakinikia makuzi yake na ya dume lake katika ulingo wa soka.

Licha ya kusutwa na wengi, baadhi ya mashabiki wake walivutiwa na picha hizo, hasa aliyopigwa akiwa anavua bikini nyeusi.

Alipakia pia picha nyingine iliyoonyesha sehemu kubwa ya maziwa yake na maeneo karibu na kitovu chake huku bikini iliyomsetiri ikikosa kuficha vilivyostahili kufichwa.

“Wewe ni mkamilifu na Luiz ana bahati kubwa sana kuwa nawe mrembo,” akaandika shabiki mwingine.

Alisha alihudumu kambini mwa Aston Villa kwa miaka mitatu kabla ya kujiunga na Juventus mwaka jana na amefungia kikosi hicho mabao mawili kutokana na mechi 15 zilizopita za Ligi Kuu ya Italia.

Asipokuwa uwanjani kutandaza boli, kidosh huyo ni mwanamitindo na mshawishi mkuu wa masuala ya burudani nchini Uswisi.

Kwa kuhamia Italia, aliungana na mpenzi wake Luiz anayechezea madume wa Juventus.

Lakini amekuwa akilalamikia pengo kubwa la mishahara yao baada ya kufichuka kuwa Luiz ambaye ni raia wa Brazil analipwa na waajiri wake Sh16.8 milioni kwa wiki, mshahara huo ulikuwa takriban mara 10 zaidi ya ule ambao Alisha anapokezwa na timu ya wanawake ya Juventus.

“Kila mtu angependa kuwa na mshahara sawa na mwenzake. Mara nyingi mimi huzungumza na Luiz nyumbani kuhusu suala hili na msimamo wangu ni kuwa hali si sawa kabisa. Ingawa tunafanya kazi sawa uwanjani, wanasoka wa kiume hulipwa takriban mara mia zaidi ya ule ujira wa wanawake. Ni jambo ambalo linaniathiri kwa sababu mimi ni mwanamke,” aliambia gazeti la La Gazzetta dello Sport.