Wahuni wavamia kanisa na kuvuruga ibada aliyohudhuria Gachagua
WALINZI wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua walilazimika kufyatua risasi hewani kuwatawanya vijana waliovamia kanisa la PCEA Kasarani East, Nairobi, Jumapili alipokuwa akishiriki ibada.
Tukio hilo liliibua taharuki katika mtaa wa Kasarani baada ya mamia ya vijana kuvamia ibada hiyo, wakidai walipwe pesa ili kushiriki hafla hiyo.
Vijana hao walivamia kanisa hilo kwa nguvu, wakaingia ndani na kuvunja viti vilivyokuwa vikitumiwa na waumini wakati wa ibada.
Wengi wa vijana hao walikuwa wamevalia sare za kijeshi na mavazi ya kivita, hali iliyozua wasiwasi miongoni mwa waumini kuhusu nia yao halisi.
Mvutano huo ulilazimisha ibada kusitishwa kwa muda, huku baadhi ya waumini wakikimbia kwa hofu ya usalama wao.

Katika vurugu hizo, gari linaloaminika kumilikiwa na Gachagua lilipigwa mawe na kuvunjwa vioo.
Habari zaidi zitafuatia..