Habari
Papa Francis aaga dunia Jumatatu ya Pasaka

Papa Francis wa Kanisa la Katoliki. PICHA|HISANI
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Papa Francis ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 88.
Kulingana na taarifa kutoka makao makuu ya kanisa hilo, The Vatican, Papa alikata roho asubuhi ya Jumatatu ya Pasaka. Ni majuzi tu alipona maradhi makali ya nimonia ambayo yalimsaza hospitalini kwa majuma mengi.
Jumapili alishiriki ibada ya Jumapili ya Pasaka ambapo alitumia fursa hiyo kuhubiri amani na upendo miongoni mwa binadamu.
Habari zaidi ni kadiri tunavyozipokea…