Habari

Kalameni ajiandalia mlo mke akitulia kwenye kifua cha mpango wa kando hotelini

Na JANET KAVUNGA April 24th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MTWAPA MJINI

JOMBI wa hapa alilazimika kujipikia asilale njaa mkewe alipomhadaa alikuwa amechelewa kazini ilhali alikuwa amelalia kifua cha mpango wake wa kando katika hoteli moja Mombasa.

Jamaa alikuwa akisubiri mkewe afike aandae chajio alipopata arafa kutoka kwa demu akimjulisha kwamba, alikuwa amechelewa kazini.

Demu alisema alipokuwa akimtumia jamaa arafa hiyo alikuwa amelala katika kifua cha dume wakijiandaa kurushana roho.

“Alikuwa mpango wangu wa kando wa kwanza na alinipandisha mizuka nikalazimika kumhadaa mume wangu. Nilifika nyumbani saa sita usiku na nikapata amepika na kula,” demu alifunguka katika ukurasa mmoja wa mtandao wa kijamii ambao akina dada huzungumzia uzoefu wa maisha ya ndoa.

***

Nilikutema kwa kulaza damu, demu aambia ex

KIRIBWET, TRANSMARA

Kipusa wa hapa alijuta kuitikia ombi la mpenzi wake wa awali la kumtaka amwambie ukweli kuhusu sababu ya kumtema.

Duru zinaarifu wawili hao walishiriki uhusiano wa kimahaba kwa muda mrefu kabla ya kipusa kumtaka jamaa ajaribu bahati kwingine.

Kipusa hakumfichulia polo sababu ya kumrusha nje lakini jamaa hakukoma kumlilia amwambie alivyokosa.

Ndiposa hatimaye kipusa alimchoma jombi kwa ukweli kuwa yeye ni goigoi kwenye tendo la ndoa.

NA KIPNGENO CHERUIYOT