Dondoo

Kisura ashindwa kufanya kazi baada kurusha roho na bosi

Na JANET KAVUNGA April 24th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MWANADADA wa hapa alishindwa kufanya kazi baada ya kurushana roho na bosi wake akihisi kuwa kila mtu katika ofisi alikuwa akijua walichepuka.

Ilibidi mwanadada huyo kuacha kazi kwa muda hadi alipopata kazi nyingine na kuapa kutomeza chambo cha wakubwa wake kazini.

“Sikuwa na amani. Nilizama katika mawazo baada ya kurushana roho na bosi wangu. Nilihisi kama kila mtu katika ofisi alifahamu uhusiano wetu. Hatimaye niliacha kazi kwa muda na nikamzima kwa simu. Baadaye nilipata kazi yangu ya sasa na nimeapa sitawahi kumeza chambo cha mkubwa wangu. Heri nikachuuze nyanya na kudumisha heshima yangu kuliko kufanya kazi ofisini na wakubwa mafisi,” demu alisimulia wenzake wakipiga gumzo katika saluni.

Jaribio la bosi huyo kumfuata kwa lengo la kufufua uhusiano huo halikufanikiwa.