Video
Wakazi wachoma lori lililogonga na kuua mama na mwanawe Namanga
WAKAZI wenye ghadhabu kando kando mwa barabara kuu ya Namanga wameteketeza lori lililogonga na kuua mama na bintiye papo hapo.
Kisa hicho kilichotokea Jumanne, Julai 15, 2025 jioni kishuhudia mama na binti yake waliokuwa wanavuka barabara katika daraja la Korompoi wakipoteza Maisha pale lori hilo lilipokosa kusimama kwa wakati.
Mara moja wakazi walilizingira na kulitia moto hata kabla ya miili kuondolewa huku ajali hiyo iliibua hamaki wakazi wakiitaka serikali kuweka matuta ili kudhibiti kasi ya magari katika kivuko hicho.