Tekinolojia inavyokidhi mahitaji ya lishe katika vyakula vilivyotayari kuliwa
Mahitaji yanayoibuka ya vyakula vilivyotayari kuliwa kwa kusindika nafaka za kiamsha kinywa zilizopikwa kwa teknolojia ya kisasa na salama, shayiri, na unga ulioboreshwa uliopikwa tayari ambao unalingana na ubora wa lishe yameongezeka.
Teknolojia hii mpya imeiweka kampuni ya Proctor & Allan (EA) Company Ltd katika nafasi ya kipekee nchini na ukanda wa Afrika Mashariki kutengeneza nafaka za kiamsha kinywa zilizosindikwa kwa teknolojia ya kisasa.
Tekinolojia hii inahusisha mchakato wa usindikaji chakula unaojumuisha kupika awali mchanganyiko wa vyakula vilivyosagwa kwa ubunifu ili kupata bidhaa tayari kuliwa.
Kwa mujibu wa kampuni hiyo, kuna ongezeko la tabaka la kati la familia nchini Kenya na ukanda mzima, zinazoangazia bidhaa za vyakula vilivyotayari kuliwa na vya urahisi.
Hali hii inachangiwa na mitindo ya maisha inayobadilika kutokana na kupungua kwa mapato ya ziada na mashindano ya muda kwa shughuli nyingi, hali inayopunguza muda wa kupika na kula.
Mkurugenzi wa Proctor & Allan EA Ltd, Stephen Nthei, aliambia Taifa Leo gazeti kwamba kampuni hiyo inalenga sehemu kubwa zaidi ya soko la nafaka za kiamsha kinywa zilizo tayari kuliwa, kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kutoa vitafunio kwa familia zaidi ya nafaka za kawaida za asubuhi.
Bw Nthei alisema pia kuwa bidhaa hizo zitatolewa kupitia njia zao za kawaida za soko na zitawapa wanunuzi chaguo zaidi. Kiwanda hicho cha kisasa kilitolewa na kampuni ya Bühler Group kutoka Uswizi kama sehemu ya mpango wa kisasa wa kampuni hiyo ili kutoa bidhaa za ubunifu.
“Familia kwa sasa zinazingatia kupata mlo kwa muda mfupi iwezekanavyo, kwa kuhamisha mzigo wa kupika kwa wingi na gharama kwa mtengenezaji, hatua inayopelekea kuwepo kwa vyakula vilivyotayari kuliwa vinavyotengenezwa kiwandani.
Wakenya wengi na Waafrika kwa jumla sasa wanatumia nafaka za kiamsha kinywa na mlo uliopikwa tayari wenye virutubisho vilivyoimarishwa, ambavyo si rahisi kupatikana katika chakula cha kawaida kwa huduma ya mara moja,”
alisema Mkurugenzi Nthei, akiongeza kuwa, “Mahitaji ya vyakula vilivyotayari kuliwa na nafaka zinazofaa kwa matumizi ya muda wote yamekuwa yakiongezeka sambamba na kupanda kwa hadhi ya Kenya kuwa nchi ya kipato cha kati, mabadiliko ya mitindo ya maisha, na mkazo wa nchi kuelekea usindikaji wa kilimo na mwelekeo wa kiuchumi wa Nunua Kenya Jenga Kenya.”