Habari
Afisa wa polisi Klinzy Barasa akanusha kumuua muuzaji barakoa Boniface Kariuki

Afisa wa Polisi Klinzy Barasa akiwa katika mahakama ya Nairobi ambapo amekanusha kumuua mchuuzi wa barakoa Boniface Kariuki wakati wa maandamano. Picha|Richard Munguti
AFISA wa Polisi wa Cheo cha Konstebo Klinzy Barasa amekanusha kumuua muuzaji wa barakoa Boniface Kariuki wakati wa maandamano ya Juni 17 kwenye barabara ya Moi Avenue, Nairobi.
Alikanusha mashtaka hayo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Kanyi Kimondo mnamo Jumatatu, Julai 28, 2025.
Mawakili wake wakiongozwa na Felix Kiton waliomba mahakama imwaachilie kwa kuwa hakuna sababu ya mno ya kuendelea kumzuilia.
Hata hivyo, Kiongozi wa Mashtaka Vincent Monda, wakili wake na Chama cha Mawakili Nchini (LSK) walipinga kuwaachiliwa kwake.
Jaji aliamuru arejeshwe korokoroni hadi Agosti 19 ambapo ombi la mawakili wake kuwa awaachiliwe kwa dhamana, litasikizwa.