Michezo

Kenya yasisimka dimba la Chan likianza

Na Michael Kirwa August 2nd, 2025 Kusoma ni dakika: 5

Kuna jambo fulani kuhusu Mashindano ya Mataifa ya Afrika (Chan)  2024 yaliyocheleweshwa kufanyika hapa Afrika Mashariki, ambalo linaendana na methali ya “mpira unarudi nyumbani”, wimbo unaohusishwa na England ikijivunia kuwa waasisi wa mchezo huu na haki ya kushinda vikombe vikubwa.

Hii ni methali ambayo pia Afrika Mashariki inaweza kumiliki huku mashindano ya bara yakianza leo Jumamosi, Agosti 2.

Mechi ya kwanza ya kimataifa ya soka kati ya nchi mbili za Afrika ilichezwa Mei 1, 1926, jijini Nairobi.

 Kenya na Uganda walitoka sare ya 1-1 kabla ya Kenya kushinda mechi ya marudio baada ya siku mbili kwa 2-1 na kushinda toleo la kwanza la Gossage Cup.

Gossage Cup, inayojulikana sasa kama Cecafa Cup, ni mashindano ya zamani zaidi ya soka ya kimataifa barani Afrika.

Ingawa sasa inahusisha timu kutoka sehemu zingine za bara, mashindano haya yalihusisha tu timu za Afrika Mashariki – Kenya, Tanzania, Uganda, na Zanzibar – hadi mwaka 1972.

Miaka 99 baadaye, Kenya, Tanzania, na Uganda zinarejesha urithi huo kwa kiwango kikubwa kwa kushirikiana katika kuandaa Chan 2024, mashindano makubwa ya CAF ambayo yatashirikisha nchi hizi tatu kuandaa mashindano hayo kwa mara ya kwanza.

Kuanzia leo hadi Agosti 30, Kenya, Tanzania, na Uganda zitakaribisha timu 16 kutoka sehemu zingine za Afrika kwa dimba la soka itakayofanyika katika miji minne ya wenyeji – Dar es Salaam, Kampala, Nairobi, na Zanzibar.

Nchi hizi tatu zinashirikiana kuandaa mashindano haya kama mazoezi ya kuandaa kwa pamoja mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) ya 2027, na maandalizi yao yameleta uboreshaji wa viwanja angalau vitano katika eneo hili.

Uwanja wa Michezo wa Kimataifa wa Moi, Kasarani na Uwanja wa Nyayo wa Kitaifa umefanyiwa ukarabati mkubwa ili kuwa tayari kwa Chan 2024.

Hali sawa ni kwa Uwanja wa Benjamin Mkapa (Dar es Salaam), Uwanja wa Nelson Mandela (Namboole, Kampala), na Uwanja wa Amaan (Zanzibar).

Nchi hizi tatu pia zinajenga viwanja vipya kama maandalizi ya kushirikiana kuandaa Afcon ya 2027, huku pia zikiboreshwa miundombinu yao ya usafiri.

Kuandaa mashindano haya pia kunatarajiwa kuimarisha utalii katika kanda hii, ambapo hoteli na biashara zinatarajia kufaidika na wingi wa wageni watakaokuja katika kanda hii.

 Wahisani wa tafsiri pia wamekuwa wakiboreshwa CV zao, wakitumaini kusaidia CAF kudumisha matumizi ya lugha rasmi za mashindano – Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, na Kireno – wakati wa mashindano ya siku 29.

Wale walio katika usafirishaji na usafiri wanajiandaa kuthibitisha uaminifu wa barabara na magari ya Afrika Mashariki. Hata ukiangalia kwa namna gani, kuna jambo kwa kila mtu.

Hata hivyo, licha ya shauku na furaha ya kukaribisha mataifa ya Afrika kwa Chan 2024, kuwa Afrika Mashariki inashirikiana kuandaa mashindano haya kuna hisia ya ndoto, hasa kwa Wakenya.

Maandalizi ya kuandaa mashindano haya yalikumbwa na mashaka na wasiwasi kuhusu uwezo wa kanda hii kutekeleza jukumu hili. Mashaka haya yalikuwa yakijikita kwenye kushindwa kwa Kenya kuandaa na kuendesha Afcon ya 1996, na Chan ya 2018. Kwamba kweli mashindano haya yanafanyika, kunatoa taswira ya kisanaa ya picha ya Salvador Dali, mambo yasiyowezekana na ya ajabu yanatokea na tunayaona.

Alhamisi asubuhi kwenye Hoteli ya Stadion wakati wa hafla iliyoandaliwa na Wizara ya Michezo na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kuwakutanisha na wachezaji wa zamani wa soka wa Kenya, Waziri wa Michezo Salim Mvurya alitangaza ushindi kwa wanaoshuku na wanaoshindana na matamanio ya wanyama wa mwituni waliovuka Mto Mara uliojaa mamba. “Mashindano yanaanza kesho nchini Tanzania na Jumapili tutacheza na DR Congo. Wakati huu imewezekana. Tunaandaa,” alisema Waziri huyo.

” Ingawa kuandaa Chan 2024  ni jambo kubwa kwa Kenya, nchi hii si geni katika bara na dunia baada ya kushinda haki za kuandaa mashindano muhimu ya michezo.

Mnamo mwaka 1987, nchi ilikuwa mwenyeji wa Michezo ya Afrika (Sasa inajulikana kama Mashindano ya Afrika). Mashindano haya yalifanyika Uwanja wa Michezo wa Kimataifa wa Moi, Kasarani, na uwanja huu, ulikuwa na watu 100,000 walioshuhudia mchuano wa Harambee Stars kumalizika na kipigo cha 1-0 kutoka Misri katika fainali.

“Baada ya mechi, tulisikia kwamba wakandarasi wa China waliokuwa wamejenga uwanja walikuwa wakizunguka uwanja kwa wasiwasi. Walikuwa wakiogopa kuwa ikiwa Kenya ingeweza kufunga bao, jukwaa hilo jipya lingeporomoka chini kutokana uzito wa watu 100,000 wakiruka kwa wakati mmoja. Labda ilikuwa bahati hatukuweza kufunga,” alikumbuka James Nandwa, aliyekuwa akichezea Kenya siku hiyo.

Hata hivyo, Kasarani ilisimama imara na mwaka 2017 na 2021, kelele za uwanja zilikuwa zikisikika duniani kote wakati Kenya ilikuwa mwenyeji wa Mashindano ya 2017 ya Michezo ya Riadha ya Dunia kwa Wachezaji Wadogo, na Mashindano ya Dunia ya Riadha kwa Wachezaji wa Umri wa Miaka 20 ya 2021. Idadi ya watazamaji ilikuwa ya ajabu kwa mashindano ya riadha ya vijana na ulimwengu uliondoka na kumbukumbu isiyosahaulika ya mapenzi ya Wakenya.

Mashindano ya Dunia ya Riadha ya 2017 yalitaja ya “mara ya kwanza nchini Kenya na mara ya mwisho duniani” kutokana na kuunganishwa na Mashindano ya Umri wa Miaka 20.

Hata hivyo, kwa Kenya, haikuwa mara ya kwanza kwa ulimwengu kuja nchini kwa mashindano ya michezo. Hii pia haikuwa mara ya mwisho.

Mnamo 2007, picha za kuchekesha za wanariadha 470 kutoka nchi 63 waliigizwa kwenye mitungi yenye maji baridi baada ya kumaliza mbio zao zilifanya dunia icheke kwa furaha huku Mombasa ikiwa mwenyeji wa Mashindano ya Dunia ya Riadha ya IAAF mwaka huo.

Miaka mitatu baadaye, bendera za nchi 46 za Afrika zilipepea kwenye Uwanja wa Nyayo wa Kitaifa wakati Kenya ikiwa mwenyeji wa Mashindano ya Afrika ya Riadha ya 2010 na wanariadha 588 walishiriki katika mashindano 44.

Miaka kumi na saba kabla, Septemba 28, 1993, mchezaji wa kikapu wa Kenya, Bush Wamukota alizaliwa siku ambayo Kenya ilimaliza ya 4 katika Mashindano ya FIBA ya Afrika ya 1993 – yaliyoandaliwa Nairobi – baada ya Morans kupoteza 76-90 katika mchuano wa kutafuta nafasi ya tatu. Kwa namna fulani, linapokuja suala la kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya michezo na kuzalisha wanamichezo, Kenya inaweza kufanya hivyo kwa siku moja.

Mashindano mengine ya michezo ya bara na kimataifa ambayo Kenya imekuwa mwenyeji ni pamoja na: Mashindano ya Riadha ya Afrika ya 1985, Mashindano ya Kuogelea ya Afrika ya 2012, Kombe la Mataifa la Hockey la Afrika la 2013 kwa wanaume na wanawake, Mashindano ya Kuinua Mizigo ya Afrika ya 2021, na mashindano kadhaa ya mpira wa mkono, raga, na voliboli kwa vijana na wazee.

Chan pia hutoa fursa kwa soka la Afrika kugundua vipaji vyake vilivyojificha na kutangaza ligi za ndani za Afrika. Mashindano haya yamezalisha nyota ambao wameendelea kung’ara katika hatua kubwa za soka barani Afrika na duniani. Wao ni pamoja na Harrison Afful (Ghana), Lamine Camara (Senegal), Nayef Aguerd (Morocco), na Patson Daka (Zambia). Wengine kama Djigui Diarra (Mali), Farouk Miya (Uganda), na wawili kutoka Rwanda, Jacques Tuyisenge na Jean-Baptiste Mugiranenza, walikuja kuwa nyota katika soka la Afrika Mashariki.

Kama wale waliotangulia, Chan inawapa wachezaji wa ndani fursa ya kutangaza majina yao katika historia ya soka ya nchi zao na bara kama vile mchezaji wa soka maarufu wa Kenya, Dennis Oliech ambaye Ijumaa alitangazwa kama balozi wa Kenya wa Chan 2024 na Waziri wa Michezo Mvurya kwenye hafla iliyofanyika Hoteli ya Stadion Kasarani.

Akikumbuka Harambee Stars katika miaka ya 1970 na 1980, Mvurya anasema kuandaa Chan 2024 ni muhimu kwa kurejesha heshima ya soka Kenya. “Soka nchini Kenya ilikuwa kila kitu. Tunataka soka nchini Kenya iwe kila kitu tena,” alisema.

Oliech, ambaye Mvurya ana matumaini atachochea Kenya na Harambee Stars kushinda kupitia jukumu lake, alikumbusha roho ya kishujaa iliyojulikana katika taaluma yake ya kitaifa kuhamasisha kikosi cha sasa cha Harambee Stars.

“Chezeni bila hofu. Msitoke uwanjani mkiwa na majuto ya kutokuwa na bidii ya kutosha,” alisema.

Nahodha huyo wa zamani wa Harambee Stars alifurahi kuona mashabiki uwanjani na hakuwahi kushindwa kutimiza ahadi yake ya kufunga bao. Hata baada ya kustaafu, ile shauku kwa umati wa mashabiki bado haijamtoka.

TAFSIRI: BENSON MATHEKA

.