Habari

Nane waangamia baada ya basi kugongwa na treni kwenye makutano

Na MWANDISHI WETU August 7th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

WATU wanane wameangamia, wengine wengi kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha treni ya mizigo na basi la Kenya Pipeline, eneo la Morendat, Naivasha.

Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Naivasha Anthony Keter, ajali hiyo ilitokea wakati basi lilipokutana ana kwa ana na treni hiyo ya mizigo katika eneo la makutano.

Basi hilo lilikuwa limebeba wafanyakazi wa kampuni ya Kenya Pipeline ambao walikuwa wametoka kituo cha mafunzo cha Morendat.

Katika taarifa, Kenya Railways imetahadhari umma dhidi ya kuvuka makutano ya reli na barabara bila kuwa na uhakika kwamba hakuna treni inayokaribia.