Habari

Maswali kuhusu jinsi mwanamume aliingia kituo cha polisi cha Kenol na kujitia kitanzi

Na MWANGI MUIRURI August 11th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

POLISI katika Kaunti ya Murang’a wanaendelea kuchunguza jinsi mwanamume aliyevalia kinadhifu alivyoingia katika Kituo cha Polisi cha Kenol kisha akajitia kitanzi.

Tukio hilo lilifanyika mnamo Agosti 5 limeibua maswali kuhusu jinsi ambavyo aliingia katika kituo hicho ambacho kinalindwa vikali kisha atamatishe uhai wake bila kutambuliwa.

Mwanamume huyo alikuwa amevalia shati jeupe, jaketi nyeusi na long’i aina ‘jeans’ yenye rangi ya kijivu.

Mkuu wa Polisi wa Murangá Kusini Charity Karimi alisema uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo na wanamakinikia pia kuna iwapo aliuawa kwingine kisha mwili ukaletwa kituoni humo kufunika waliohusika.

Wakati huo huo, Rais William Ruto ameahidi kuzindua ujenzi wa barabara kuu ya Rironi-Mau Summit-Malaba hapo Oktoba akielezea matumaini kuwa mradi utarahisisha uchukuzi hadi magharibi mwa Kenya na kuchochea maendeleo.

Akiongea jana, alipohudhuria ibada katika eneobunge la Limuru, Dkt Ruto alielezea matumaini kuwa mradi huo utakamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.

“Itakuwa barabara ya safu mbili kuanzia Kamandura hadi Naivasha. Itakuwa na safu sita, kuanzia Naivasha hadi Nakuru na hatimaye Malaba,” rais akaeleza alipowahutubia waumini katika Kanisa la PCEA Joshua Matenjwa Memorial.

“Hapa Kiambu pekee tunajenga jumla ya nyumba 15,000 za gharama nafuu na tumewekeza Sh40 bilioni kufadhili miradi ya ujenzi wa barabara. Isitoshe, tumetanga Sh4.3 bilioni za kufadhili ujenzi wa makosa 18 ya kisasa,” Dkt Ruto