• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:05 AM
Jeshi la Uingereza lanunulia vifaa timu ya mtaani, Kiambu

Jeshi la Uingereza lanunulia vifaa timu ya mtaani, Kiambu

Na LAWRENCE ONGARO

KLABU ya Malezi Mema Foundation, imepokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa maafisa wa  jeshi la angani la Uingereza.

Kocha wa kikosi hicho Tiobath ‘Alpha’ Mugiira, na naibu wake Sammy ‘Rooney’ Kioko, wamekuwa wakiwanoa vijana hao wadogo katika uwanja wa shule ya msingi ya Kasarini, mjini Kiambu.

Mnamo Jumatano jioni katika uwanja wa Kasarani kikosi cha kutoka Uingereza cha Royal Air Force kilizuru uwanja huo kikiwa na zawadi tele ya vifaa vya michezo kwa timu hiyo.

Ujumbe wa watu kumi ulizuru Kiambu ili kujionea wenyewe jinsi vijana wadogo wanavyoonyesha vipaji vyao wakiwa wadogo.

Ujumbe huo pia inazuru nchi zingine za Afrika ili kujionea wenyewe jinsi vijana wadogo wanavyojibidiisha kusakata soka..

Tayari wamezuru maeneo mengine ya jiji la Nairobi kama Mathare, Kibagare, na Githorogo, huku lengo lao kuu likiwa ni kusaidia vijana hao na vifaa muhimu vya soka na kutoa mawaidha inayostahili.

Malezi Mema Foundation ya Kiambu wakati wa kupokea vifaa vya michezo kutoka kwa ujumbe wa Royal Air Force ya Uingereza, katika uwanja wa Kasarani, Kiambu. Picha/ Lawrence Ongaro

Baadhi ya vifaa vilivyokabithiwa vijana hao ni mipira, jezi suruali fupi, na vifaa vingine vya kufanyia mazoezi uwanjani.

Watoto hao walionyesha furaha kubwa baada ya kupokea vifaa hivyo huku wakionyesha wazi kuwa wako tayari kupiga hatua zaidi katika mazoezi yao.

Wageni hao kutoka Uingereza wamejitolea kuzuru Kenya na nchi zingine muhimu za bara Afrika kwa lengo la kuinua soka kutoka mashinani.

Mmoja wa mshirikishi mkuu aliyefanikisha ziara hiyo kufana ni Irene Nyambura, ambaye alihakikisha ujumbe huo unazuru Kiambu na kujionea hali ya soka ya vijana wadogo.

Kinara wa ujumbe huo ambaye ni mmoja wa afisa wa jeshi la Royal Air Force Uingereza Bw Neil Hope, alisema wamefurahia kujionea wenyewe vijana wadogo wakionyesha vipaji vyao.

“Hii ni mara yetu ya kwanza kuzuru Kenya na tumeridhika na jinsi hali ya soka imepiga hatua kubwa hasa kwa vijana wa umri mdogo. Tutazidi kufadhili vijana hao na kuhakikisha wamepiga hatua katika kiwango kingine,” alisema Bw Hope.

Alisema watazidi kuwasaidia vijana hao wadogo kwa sababu ni vyema kukuza talanta yao na kuwainua kimaisha.

Tayari watazuru vilabu kadha za hapa nchini hasa za mashinani katika jiji la Nairobi, lengo likiwa kutoa misaada na kutoa mawaidha jinsi ya kupiga hatua zaidi.

You can share this post!

Mshubiri kwa Valentino Dei ya OCS wa zamani kuhukumiwa...

Napenda mbinu za Sarri, asema Hazard licha ya kumumunywa...

adminleo