Balozi wa Uingereza afunganya virago
BALOZI wa Uingereza nchini Neil Wigan OBE amesema wakati wake wa kuhudumu nchini utakamilika Agosti hii ambako anatarajiwa kurejea kwao.
Hii ni baada ya Uingereza, Jumatatu kusema kuwa miaka miwili ya Wigan itakuwa inatamatika Agosti na atapokezwa majukumu mengine.
“Uhusiano kati ya Kenya na Uingereza umeimarika kwenye nyanja za kibiashara, teknolojia, ubunifu na utamaduni ambao unanufaisha nchi zote mbili,” akasema Balozi Wigan.
Kipindi cha miaka miwili alichokuwa nchini kilishuhudia Kenya ikitembelewa na wageni mashuhuri kutoka Uingereza akiwemo Mfalme Charles 111 na kutiwa saini kwa mikataba ya uwekezaji kwenye miundomsingi kama Reli ya Nairobi na mafunzo kwa wanaofanya kazi kwenye sekta ya usafiri wa majini.