Habari

Elachi pabaya baada ya kubwagwa katika kura ya ODM

Na WINNIE ATIENO August 18th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MBUNGE wa Dagoretti Kaskazini Beatrice Elachi anapambana kusalia na ushawishi ndani ya ODM baada ya kubwagwa kwenye kura ya kuwa mwenyekiti wa chama katika eneobunge hilo.

Bi Elachi alibwagwa na Diwani wa Kilimani Moses Ogeto ambaye amekuwa katika siasa za jiji kwa kipindi kirefu.

Uchaguzi huo wa mashinani ulirudiwa baada ya kuzuka kwa tofauti kali kati ya kambi za Bi Elachi na diwani huyo mwenye ushawishi mmkubwa Dagoretti ambaye pia anamezea mate kiti hicho 2027.

Bi Elachi alisema uchaguzi wa Alhamisi ulijaa hila na udanganyifu na baadhi ya wajumbe walizuiwa kupiga kura.

Hata hivyo, kambi ya Bw Ogetto imemtaka akubali kuwa alishindwa na aunge mkono viongozi wa sasa.