Habari

Polisi wasaka mwili wa binti anayesemekana kuuawa na mpenziwe na kuzikwa pangoni

Na WYCLIFFE NYABERI  September 4th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MAAFISA wa polisi kwa ushirikiano na wenzao kutoka Wizara ya Afya wanaendelea na shughuli za kuufukua mwili wa binti mmoja anayesemekana kuuwawa na mpenziwe na kisha kuzikwa kisiri katika pango moja kijijini Maosi, Nyamaiya, Kaunti ya Nyamira.

Mwili wa Faith Kemunto, 20, unasemekana kuwa katika pango hilo baada ya familia yake kupokea habari kuhusu kifo chake kutoka kwa mpenzi huyo kupitia arafa ya simu.

Maafisa wa polisi kwa ushirikiano na wenzao kutoka kwa Wizara ya Afya katika harakati za kusaka mwili pangoni. Picha|Wycliffe Nyaberi

Mpenzi huyo ambaye ametambuliwa kama Gideon Makori, anasemekana kumuua Bi Kemunto mwezi mmoja uliopita baada ya kumtorosha kutoka kwa wazazi wake.

Kwa kipindi hicho alichotoroka na binti huyo, jamaa huyo alihakikisha Kemunto hawasiliani na wazazi wake kwa kumpokonya simu yake.

Lakini ilipofika Jumapili iliyopita, jamaa huyo aliwaandikia arafa jamaa wa Bi Kemunto kuwafahamisha kuwa alikuwa amemuua na kumzika kisiri.

Mwili wa Faith Kemunto, 20, unasemekana kuwa katika pango hilo baada ya familia yake kupokea habari kuhusu kifo chake kutoka kwa mpenzi wake kupitia arafa ya simu. Picha|Wycliffe Nyaberi

Pia katika maelezo hayo ya arafa, jamaa huyo anadaiwa kueleza mahali ambapo alimzika.

Bi Kemunto alifaa kujiunga na Chuo Kikuu cha Machakos mwezi huu wa Septemba.

Habari zaidi kufuatia….