Jamaa aanika uchu kwa mke wa rafikiye akiwa mlevi
SHANZU, MOMBASA
KALAMENI wa hapa alijipata pabaya kwa lushindwa kujizuia na kuanza kumezea mate mke wa rafiki yake wa karibu.
Juzi, akiwa amelewa, jombi alimnong’oneza rafiki yake maneno yaliyomchemsha. “Eeeh bro, si kwa ubaya lakini bibi yako ni bonge la mali. Haki ameiva poa!”.
Maneno hayo yalimkera rafikiye ambaye alimuita pembeni na kumuonya vikali asiwahi kurudia kauli kama hiyo.
“Kama ni ulevi umekupanda hadi unatamani mke wangu, ujue urafiki wetu unaisha leo,” rafiki huyo alimwambia kwa hasira.
Hali hiyo ilisababisha mtafaruku mkubwa baina ya marafiki hao wawili, huku mke wa jamaa akidai kuwa jombi huyo alikuwa ameanza kumtumia jumbe tata.