Mwanahabari aliyeripoti chanzo cha Covid-19 asukumiwa miaka 4 zaidi jela
MWANAHABARI aliyefungwa jela baada ya kuangazia awamu za awali za mlipuko wa Covid-19 alihukumiwa nyongeza ya miaka minne gerezani Ijumaa, lilisema shirika la Reporters Without Borders.
Zhang Zhan, 42, alihukumiwa kwa shtaka la “uchokozi na kuchochea balaa” nchini, shtaka lile lile lililosababisha afungwe jela Disemba 2020 baada ya kuchapisha masimulizi ya moja kwa moja kutoka jiji la Wuhan kuhusu mwanzo wa kusambaa kwa virusi vya corona, kundi la kimataifa kuhusu uhuru wa vyombo vya habari linalofahamika kwa anwani zake za Kifaransa RSF, lilisema Jumamosi.
Waziri wa Masuala ya Kigeni nchini hakupatikana jana kuzungumza. Reuters haikuweza kubaini iwapo mwanahabari huyo ambaye ni raia nchini alikuwa na wakili.
“Anafaa kusherehekewa kote duniani kama “shujaa wa habari,” sio kuzuiliwa katika mazingira ya kikatili ya gereza,” Msimamizi wa RSF Bara Asia, Aleksandra Bielakowska, alisema katika taarifa.