Makalameni wararuliana mashati kugundua walikuwa wakichovya kwenye buyu moja
MAKUPA, MOMBASA
MAKALAMENI wawili mtaani hapa walichangamkiana baada ya kugundua walikuwa wakitoka na demu mmoja, binti mrembo aliyekuwa akiwasambazia asali bila wao kujua.
Kwa muda mrefu, wawili hao walikuwa wakitembea kifua mbele mitaani, kila mmoja akijiona ndiye mwenye bahati ya kumwingiza boksi kipusa huyo bila kujua alikuwa hodari wa kupanga wanaume.
Lakini juzi, ukweli ulijitokeza wazi mmoja alipokuwa akingojea demu jioni karibu na kwake mwanadada alipofika akiwa na polo mwingine.
Wakiwa bado wanatazamana kwa mshangao na mshtuko, binti aliangua kicheko huku wanaume hao wakianza kutaniana.
“Wee bro, kumbe umekuwa ukinigongea?” Jamaa aliyekuwa akisubiri demu alianza. Mwenzake alimjibu kwamba wote walikuwa wakigongeana kisha wakaangua kicheko na kukumbatiana.