Dondoo

Lofa aliyeiba chupa ya pombe anunuliwa kreti amalize

Na DENNIS SINYO October 7th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

KOCHOLIA, TESO

MWANAMUME aliyekamatwa baada ya kufumaniwa akiiba chupa ya pombe alikuwa na wakati mgumu baada ya wateja kumnunulia kreti nzima ya pombe.

Inasemekana walinzi wa baa walimkamata akiiba pombe ya mteja aliyekuwa ameenda msalani kujisaidia.Jamaa ambaye ni lofa wa mtaa alianza kulia akiomba msamaha.

Alidai licha ya kuwa mraibu,hakuwa ameonja dozi wiki nzima. Kilio chake kilivutia wateja kwenye baa hiyo wakaamua kuchanga pesa na kumnunulia kreti nzima ya pombe.