Dondoo
Mwanasiasa mkono gamu apapurwa vikali kutembelea wafiwa kijijini mikono mitupu

MAVUENI, KILIFI
MWANASIASA mmoja wa hapa alikosolewa vikali kwa kutembelea familia ya marehemu mikono mitupu.
Ingawa alikusudia kutoa pole kwa familia, kitendo hicho kilionekana kama cha kutokuwa na utu, huku wengi wakisema alipaswa kuleta msaada wa kifedha au vinginevyo kufariji familia ambayo ilikuwa na wakati mgumu kuandaa mazishi ya mpendwa wao.
Wakazi walimlaumu kwa kujitokeza wakati wa misiba ili kujenga uhusiano na umma.
Walidai alitumia familia hiyo kama sehemu ya kujitangaza badala ya kuisaidia wakati wa dhiki.