Habari za Kaunti

Mbunge alalamikia ongezeko la shule za kibinafsi

Na WINNIE ATIENO October 10th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MBUNGE wa Mvita, Mohamed Soud amelalamikia ongezeko la shule za kibinafsi, katika eneobunge lake akionya kuwa hali hiyo inatishia shule za umma.

Mbunge huyo alisema ana wasiwasi kuwa kuongezeka kwa ghafla kwa shule za kibinafsi katika eneobunge lake kumefanya shule za umma kusalia bila wanafunzi licha ya serikali kuwekeza kwa manufaa ya wakazi.

Alitaja shule ya msingi ya Serani ambayo serikali iliwekeza ili kuongeza idadi ya wanafunzi kama mfano wa inayoathiriwa.