Shangazi Akujibu

SHANGAZI AKUJIBU: Mpenzi ana mimba ya mtu wake wa zamani

Na SHANGAZI October 22nd, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Nilikutana na mpenzi wangu miezi kadhaa baada ya kuachana na mpenzi wake. Amegundua ana mimba ya mwanamume huyo na anataka kuitoa kwani anaofia sitaweza kumpenda mtoto huyo. Waonaje?

Jibu: Mpenzi wako amekwambia ukweli ili umshauri na uamuzi wake unategemea ushauri wako. Kama unampenda na uko tayari kumlea mtoto huyo kama wako, mwambie hivyo ili kumuondolea hofu. Kama huwezi mwambie pia.