Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Mzee ana akaunti ya siri

SWALI: Nimegundua mzee ana akaunti ya siri ya benki
Shangazi, nilishangaa sana nilipogundua mume wangu ana akaunti ya siri benki. Nifanyeje?
Jibu: Usianze vita. Kaa naye na umuulize kwa utulivu kwamba hupendi hiyo tabia yake. Hata hivyo, huenda anachukua tahadhari ya kifedha kwa manufaa ya familia au huenda tu ikwa dalili ya ukosefu wa uaminifu.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO